Jinsi ya Kuweka Password Kwenye USB Flash Drive Yoyote Written by Am IT guy STEPADO Ni kweli kwamba hivi sasa karibia kila kitu kina kuja na uwezo au sehemu ya password, lakini kuna baadhi ya vifaa ambavyo sio vya kisasa na havina sehemu maalum ambayo unaweza kuzima na kuwasha password kwa urahisi. Kuliona hili leo Solution Tech tunakuletea njia rahisi ambayo unaweza kuweka password kwenye USB Flash Drive yoyote kwa urahisi na haraka. Njia hizi zinaweza kufanyika pale unapokuwa na kompyuta hivyo hakikisha unayo kompyuta kabla ya kuendelea kwenye hatua hizi. Basi bila kupoteza muda twende kwenye hatua hizi moja kwa moja. Kwa Kutumia Njia ya BitLocker BitLocker ni sehemu ambayo inapatikana kwenye kompyuta zote zenye mfumo wa Windows 10, sehemu hii inaweza kusaidia kuweka password kwenye USB Flash yoyote kwa urahisi na haraka. Kama unataka kuweka password kwenye USB Flash kwa kutumia sehemu ya BitLocker, unacho takiwa kufanya ni kuchomeka Flash yako kwenye kompyuta kisha moja kwa moja ing...