Written by Stepado Pascal Futa Vitu Kwenye Recycle Bin Unapozima Kompyuta Kuna wakati mtu unakuwa na haraka ya kutumia kompyuta yako kiasi kwamba unasahau kufuta vitu kwenye recycle bin ya kompyuta yako, kupitia njia hii leo nitakuonyesha njia ambayo unaweza kutumia ili vitu vilivyopo kwenye recycle bin vijifute vyenyewe pale unapozima kompyuta yako. Kabla ya kuanza labda nikueleze ni maana ya Recycle bin, kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta kwa muda mrefu basi lazima unajua sehemu hii, kama wewe ni mgeni wa kutumia kompyuta basi ni vyema ufahamu kuwa sehemu hii ni ile ambayo ukifuta kitu kinahifadhiwa humo kwaajili ya kusubiria kufutwa kabisa au kuondolewa moja kwa moja kwenye kompyuta yako. Sasa lengo la maujanja ya siku ya leo ni kusaidia kufuta vitu vilivyomo kwenye Recycle bin pale tu unapozima kompyuta yako, njia hii itakusaidia zaidi kama kompyuta yako ina nafasi ndogo kwani hiitasaidia kuondoa baadhi ya mafile ambayo hayana kazi au hayatumiki tena. Pia kwa kut...