Written by Stepado Pascal
Futa Vitu Kwenye Recycle Bin Unapozima Kompyuta
Kuna wakati mtu unakuwa na haraka ya kutumia kompyuta yako kiasi kwamba unasahau kufuta vitu kwenye recycle bin ya kompyuta yako, kupitia njia hii leo nitakuonyesha njia ambayo unaweza kutumia ili vitu vilivyopo kwenye recycle bin vijifute vyenyewe pale unapozima kompyuta yako.
Kabla ya kuanza labda nikueleze ni
maana ya Recycle bin, kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta kwa muda mrefu basi
lazima unajua sehemu hii, kama wewe ni mgeni wa kutumia kompyuta basi ni vyema
ufahamu kuwa sehemu hii ni ile ambayo ukifuta kitu kinahifadhiwa humo kwaajili
ya kusubiria kufutwa kabisa au kuondolewa moja kwa moja kwenye kompyuta yako.
Sasa lengo la maujanja ya siku ya
leo ni kusaidia kufuta vitu vilivyomo kwenye Recycle bin pale tu unapozima
kompyuta yako, njia hii itakusaidia zaidi kama kompyuta yako ina nafasi ndogo
kwani hiitasaidia kuondoa baadhi ya mafile ambayo hayana kazi au hayatumiki
tena.
Pia kwa kutumia njia hii itakusaidia
kama unatumia kompyuta ambayo sio ya kwako, kwani hii itakusaidia kufuta vitu
vyote ambayo ulifuta wakati unatumia kompyuta hiyo ambayo pengine uliazima.
Lakini pia kama unatumia Recycle bin
kama sehemu ya kuficha vitu basi njia hii haitokuwa muhimu sana kwako kwani
itafanya upoteze mafile yako yote. Basi baada ya kusema hayo twende tukangalie
njia hizi.
Kwa kuanza ingia kwenye Desktop yako
kisha fungua application ya Notepad kisha copy na paste code hizo hapo chini
kwenye ukurasa huo wa Notepad. Bofya hapo chini kucopy code hizo.
Baada ya hapo badilisha format ya .txt
na kisha weka .bat alafu Save code hizo kwenye kompyuta yako. Baada ya
hapo bofya mara mbili code hizo na utaona vitu vilivyopo kwenye Recycle bin
vimefutika, kama havija futika basi angalia labda kuna kitu umekose rudia tena
kwa kufuata maelezo kwa usahihi zaidi.
Hakikisa file linasomeka kwa mfano kufuta.bat
na sio kufuta.txt, baada ya kufanya hatua hizo hapo juu sasa nenda
kwenye sehemu ya ku-search kwenye kompyuta yako kisha andika “gpedit.msc” bila
alama za funga na fungua semialafu bofya enter kwenye keyboard yako.
Baada ya hapo litafuguka jedwali
lenye jina Local group policy editor, kuwa makini na sehemu hii kwani
hapa ndipo panapo endesha kompyuta yako nzima. Baada ya kufungua jedwali hili,
upande wa kushoto chagua Windows Settings, kisha utaona page nyingine
imefunguka tena kwa chini, Tafuta sehemu iliyo andikwa Scripts
(Startup/Shutdown), bofya hapo mara mbili kisha chagua Shutdown kwa
kubofya mara mbili.
Baada ya hapo ukurasa mwingine
utafunguka kisha bofya sehemu ya Add kwenye kibox alafu bofya Browse
kisha chagua mahali ulipo hifadhi zile code zenye jina kwa mfano kufuta.bat
kisha bofya Open. Baada ya hapo utakuwa umemaliza zoezi zima na sasa
utakuwa upo tayari kufuta mafile yako kwenye recycle bin kila mara unapozima
kompyuta yako.
Hiyo ndio njia rahisi unayoweza
kutumia pale unapotaka kufuta mafile kwenye recycle bin kwa haraka Zaidi.
Kama kuna mahali umekwama au
hujaelewa unaweza kuuliza kupitia sehemu ya maoni hapo chini nasi tutakujibu
kwa haraka.
Solutions Tech tumejikita
kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi tufuate
kwenye mitandao
Comments
Post a Comment