Skip to main content

Antivirus ipi Bora zaidi kwa Windows 10?

Welcome in Technology  MAADA LEO*Anti-virus Ipi ni Bora zaidi kwa Windows 10?* *By Am IT guy STEPADO*Windows 10 haitaingilia kazi mara kwa mara kukutaarifu kupakia ‘Anti-virus’ kwenye mashine yako kama vile Windows 7 ilivyokuwa ikifanya. Hii ni kwa sababu kuanzia Windows 8, Microsoft walifanya uamuzi wa msingi wa kuweka Anti-virus moja-kwa-moja kwenye mfumo wao. Antivirus hii inaitwa Windows Defender na ni Antivirus ambayo Microsoft wenyewe wanaitoa bure pamoja na WIndows mpya. Kwa maana hiyo swali la msingi la makala hii linafaa kubadilika na kuwa – ‘Je Windows Defender ni antivurus ni bora zaidi kwa usalama wa kompyuta yako au la?’
Windows DefenderWIndows Defender inatokana na Microsoft Security Essentials (MSE) na ni, kwa maneno mengine, toleo la kisasa zaidi la MSE, ambayo ilikuwa ni antivirus ya bure kabisa kwa ajili ya Windows 7. Kwa sasa, antivirus ya Windows Defender inakuja pamoja na Windows na ni ngome ya kwanza kwa kompyuta yako.*Je, Windows Defender Inatosha?*Unapoanza kutumia Windows 10, Windows Defender nayo huanza kufanya kazi moja-kwa-moja na ku-scan kila programu unayofungua na kwa mpangilio wa kawaida, inaji-sasisha yenyewe unapojiunga na mtandao. Kwa kawaida Windows Defender haionekani wazi ikifanya kazi ila unaweza kupata ripoti ya kina zaidi ya usalama wa kompyuta yako ukitaka kwa kuifungua Windows Defender, kwa kuitafuta kwenye orodha ya programu zako kwenye ‘Start Menu’.ximg_55c4e51e37203.png.pagespeed.ic.41bLR7DqOHKiujumla, watalamu wengi mtandaoni husema kwamba anti-virus za Microsoft zipo nyuma kidogo ya nyingine zenye ushindani, hata-hivyo, Windows Defender ina faida lukuki.Defender inakuja moja-kwa-moja na Windows na inafanya kazi kimya-kimya (haina usumbufu wa matangazo mara kwa mara) na haitumii rasilimali nyingi. Pia, haitatumia data zako za kwenye kivinjari, zinazotumika kujaribu kutengeneza faida kama vile inavyofanywa na makampuni mengine yanayotoa antivirus bure.Windows Defender siyo mbaya sana kwa usalama kompyuta yako iwapo ukizingatia mambo machache kama kusasisha kompyuta na kivinjari chako na pia kuepuka kutumia programu hatarishi kama kiwezeshaji cha java (‘java plugin’).Kwenye matokeo ya AV-Test, Windows Defender ilipata 0.5 / 6 kwa usalama, huku ikikamata 95% ya virusi na programu hatarishi (“widespread and prevalent malware”) mnamo June mwaka huu, pamoja na 85% ya virusi vya siku hadi siku. Ukilinganisha, BitDefender iliweza kakamata asilimia 100 na 100 ya sampo, huku Kaspersky ikikamata asilimia 100 na 99. Kwa mantiki hiyo, pamoja na utofauti kati ya matokeo hayo, Windows Defender bado ina usalama wa kuaminika. Microsoft wenyewe wamekuwa wakisikika wakiweka wazi kwamba dhumuni lao ni kushughulika na programu hatarishi na virusi vinavyoathiri kompyuta nyingi na ni tofauti na watengenezaji wa antivirus ambao wanashindana na virusi vya kila siku na hivyo kujiweka katika mazingira mazuri ya kushinda majaribio yoyote.ximg_55c4e503210a0.png.pagespeed.ic.HYhbdhagbIWindows Defender kwenye chaguzo za Usalama wa Windows 10WIndows 10 pia ina usalama wa aina tofauti pia, ambao ulianza kutumika katika Windows 8 kama SmartScreen filter ambayo inakuzuia kushusha na kupakia programu hatarishi, hata kama ukitumia antivirus tofauti na ya Microsoft. Chrome na Firefox nazo huwa na ‘Google’s Safe Browsing’, ambayo inakuzuia kushusha programu hatarishi.Kiujumla, Windows Defender inaweza kuwa sawa tu kwa watumiaji wa kawaida. Hili ni pamoja na kuzingatia hatua chache za kujilinda. Ilani lakini, kama wewe ni mtumiaji wa programu ambazo siyo kutoka vyanzo vya kuaminika (kama torrent) na unafanya mambo mengine hatarishi kwa kompyuta yako, unashauriwa kutafuta antivirus nyingine yenye uwezo zaidi.Tumia MalwareBytes Anti-Exploit PiaKama ziada unashauriwa sana kutumia programu maalumu ya kuzuia mashambulizi yanayoelekezwa kwenye kivinjari na visaidizi vyake. Hivi hulengwa sana na wadukuzi wa mtandao. MalwareBytes Anti-Exploit ni mfano wa programu kama hii, na ni ya bure ambayo unashauriwa kutumia. MalwareBytes kazi sawa na programu ya Microsooft iitwayo EMET security tool, lakini ina utofauti wa kuwa rahisi zaidi kutumia na ina vipengele vingi zaidi vya usalama. Hizi zana zinasaidia kuzuia mbinu nyingi zinazojulikana za ki-udukuzi. MalwareBytes Anti-Exploit inaweza kuzuia hata yale matatizo ya kiusalama ya Adobe Flash yanayosikika mara kwa mara.MalwareBytes Anti-ExploitMalwareBytes Anti-ExploitWindows Defender ikitumika sanjari na MalwareBytes Anti-Exploit ni suluhisho tosha na la nafuu unaloshauriwa kutumia kufanya kompyuta ya mtumiaji wa kawaida wa Windows 10 kuwa salama. Watu wanaotumia Windows 10 kwenye kompyuta za kiofisi zaidi wanaweza kuweka Windows Defender ikishirikiana na Microsoft EMET, ila Windows defender na MalwareBytes Anti-Exploit ni njema zaidi kwa kompyuta za kawaida. MalwareBytes Anti-Exploit pia inaweza kutumika na anti-virus nyingine yoyote na itakamata programu hatarishi na programu nyingine ambayzo hazihitajiki (zinazolazimisha kujiweka zenyewe) na zile ambazo anti-virus huwa hazikamati.INAYOHUSIANA  TB 2 - USB Flash Drive yenye ujazo mkubwa zaidi yatambulishwa!Lakini Antivirus Ipi Ni Bora zaidi?Sawa, labda hauja-ielewa Windows Defender sana na unataka kitu kingine chenye jina kubwa.Kwenye swali hilo kuna majibu mawili: Kama unatafuta anti-virus ya kulipia, Kaspersky na BitDefender kwa kawaida huwekwa kati ya anti-virus 3 nzuri zaidikatika majaribio mengi ya antivirus.Kama unatufuta antivirus ya bure, Windows Defender bado ni jibu tosha. Bado kama moyo wako unaenda kwenye anti-virus nyingine unazojua za bure, hakikisha antivirus hizo haziweki kitu kwenye kivinjari chako au kukuwekea programu nyingine amabazo pengine hupendi au hutumii. Hivi vyote huwekwa ili kulipia kile wanachosema kwamba ni bure (hakuna kitu cha bure aisee, ni ujanja tu). Wanalipaje? Wanatumia data zinazopatikana kwa wewe kutumia programu hizo zinazojilazimisha kwenye kivinjari au kompyuta yako – kwa maneno mengine, wanauza data kuhusu unatumiaje programu hizo.Windows Defender itaacha kufanya kazi unapoweka anti-virus nyingine kutoka kampuni tofauti na Microsoft na kujirudisha tena pale unapotoa anti-virus tofauti. Windows Defender imetengenezwa kutokubughudhi.Neno la MwishoKwa antivirus yoyote utakayoweka, tegemea kwamba hautakuwa salama asilimia 100. Kama umezoea kushusha na kupakia programu hatarishi, ipo siku utaingia matatani. Kuweka antivirus bora ni jambo la kukupa amani kwamba uko salama ila kama haufuati taratibu za matumizi salama ya kompyuta – ni kazi bure. Na katika dunia ambayo, kirusi cha kuogopa zaidi ni kile kisichojulikana kabisa kile kinacholenga kivinjari, MalwareBytes Anti-Exploit inaweza kuwa kimbilio bora zaidi kwa usalama wa kompyuta ya Windows 10 kuliko kukimbilia antivirus nyingine zaidi ya Windows Defender.

x

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kusoma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online

  Jinsi ya Kusoma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online Written by Stepado Pascal Ni wazi kuwa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia kuna sababu nyingi sana ambazo zinaweza kukufanya uwe na uhitaji wa kusoma meseji uliyotumiwa kupitia programu ya WhatsApp bila programu hiyo kuonyesha kama upo “online” au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo. Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia mpya na rahisi ambayo unaweza kutumia ili kujibu meseji zako za WhatsApp unazotumiwa bila programu ya WhatsApp kuonyesha kama upo online au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo yaani tiki mbili za blue. Najua kila mtu anaweza kusema najua hiyo lakini nakushauri endelea kusoma makala hii hadi mwisho kwani unaweza kupata maujanja mapya ambayo pengine ulikuwa hujui kwa namna moja ama nyingine. Kama kawaida sipendi kupoteza muda wako mwingi kwa maneno yangu, basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia ya kwanza. Njia ya Kwanza Najua kuwa unaweza kusema kuwa unaweza k...

Download Programu ya Microsoft Office 2019 Pro Plus

Download Programu ya Microsoft Office 2019 Pro Plus Written by STepado pascal Ikiwa tunazungumzia programu bora kwaajili ya ofisi ni wazi kuwa programu ya Microsoft Office ni programu bora sana kwako, programu hii inakuja na uwezo mkubwa sana wa kusaidia mtu ambaye anafanya kazi kwenye ofisi, au hata kama wewe ni mwanafunzi programu hii ni bora sana kwako. Kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia sana kuweza kupata programu ya Microsoft Office 2019 Pro Plus, ambayo imesheheni sifa nyingi sana bure bila kulipia gharama yoyote. Kumbuka hili ni toleo la Pro Plus hivyo limesheheni sifa zote za programu ya Microsoft Office. Baadhi ya programu ambazo zipo ndani ya toleo hili ni pamoja na –     Microsoft Word     Microsoft Excel     Microsoft Powerpoint     Microsoft Outlook     OneNote     OneDrive     Microsoft Teams Kwa kuanza ni vyema kufahamu kuwa programu hii ni kwa ajili ya kompyuta za Windows na inafany...

Kuanzia A-Z List zote za Windows CMD Commands

A-Z List 0f Windows CMD Commands  By  Am IT guy STEPADO Zifuatazo ndizo   list zote za Windows CMD commands  ambazo nimezipangilia katika alphabetically CMD commands. Command Prompt  and  CMD Commands  are unknown territories for most of the Windows users, they only know it as a black screen for troubleshooting the system with some fancy commands. repair a corrupted disk, hide certain drives, to create a hacking-like environment, etc. Nini maana ya Command Prompt na CMD Commands? Command Prompt, kwa jina jingine ni  cmd.exe  or  cmd  —   ni  command line amabyo inatumika kutafsiri application  katikaWindows NT family operating systems. Na CMD Commands ni specific set of instructions given to Command Prompt to perform some kind of task or function on your Windows PC. Most of the Windows CMD Commands are used to automate tasks via script  and batch files, perform advanced administrative functi...

Jinsi ya Ku-install Windows 10, 8, 7 na XP Kwenye Simu za Android

 Jinsi ya Ku-install Windows 10, 8, 7 na XP Kwenye Simu za Android Written by STepado Pascal windows kwenye android (1) Kutokana na teknolojia kubadilika sana vile vile hata simu zetu nazo zimekua zikibadilika kila siku, simu zetu zimekuwa zimebadilika kuanzia uwezo, vitu inavyofanya mpaka matumizi ya simu hizo. kuelewa mabadiliko hayo leo Tanzania Tech tunaenda kukuonyesha njia rahisi ya kuinstall Windows 7, Windows 8, Windows 10 pamoja na Windows XP kwenye simu yako ya Android. Kwa kuanza ni vyema ukajua kuwa uwezo wa kutumia Windows kwenye simu yako unaweza kukusaidia wewe kutumia simu yako kama kompyuta, njia hii itakusaidia sana kama simu yako inauwezo wa kutumika kwenye screen kubwa ili kukupa uwezo wa kufanya vitu mbalimbali kama unavyo tumia kwenye kompyuta, yaani bila tofauti kubwa utafauti ni kwenye graphics pekee. Kwa kuanza unatakiwa kuwa na simu yako ya Android yenye RAM at-list GB 1 na kuendelea, uharaka wa kuinstall Windows kwenye simu yako unategemeana sana na Uwezo...

Njia za Kutoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki (Njia Rahisi)

Njia za Kutoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki (Njia Rahisi) Written by Stepado Pascal Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanakuwa na tatizo la simu yako kustaki mara kwa mara basi makala hii ni kwa ajili yako. Kama unavyojua, simu nyingi za Android za sasa zinakuja zikiwa zimefungwa moja kwa moja na hauwezi kufunguka simu hiyo kwa namna yoyote. Ni kweli kwamba njia rahisi ya kuweza kuondoa simu kwenye hali ya kustaki ni kutoa battery ya simu hiyo na kurudisha, lakini unafanyaje kama simu yako imefungwa moja kwa moja na huwezi kufungua simu hiyo ili kutoa battery...? Majibu ninayo. Kwanza awali ya yote labda nikwambie kuwa, hatizo hili limenikuta binafsi na katika hali ya kufanya ufumbuzi nikaona sio mbaya nikishiriki na wewe njia ambazo nilitumia kuweza kuondoa simu yangu kwenye hali ya kustaki. Kumbuka njia hizi mara nyingi zinafanya kazi kwenye simu za aina zote yaani simu za Android pamoja na simu za iPhone au iOS.Zipo njia nyingi sana lakin katika zote...

Link ya kupata windows

Mambo vp Wana blog ,leo nimekuletea link hii hapa chini ,uweze kupakuwa window yoyote uitakayo kwa matumizi yako ,hvo basi bila kupoteza wakati click hiyo link hapo itakupeleka kupakuwa windows. Ukipata changamoto yoyote niachie comments yako hapo chini au chochote Cha kushare nasi karibu Sana.Tukutane tena wakati mwingine Click hapa