Jinsi ya Kusoma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana
Online
Written by Stepado Pascal
Ni wazi kuwa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia kuna sababu nyingi sana ambazo zinaweza kukufanya uwe na uhitaji wa kusoma meseji uliyotumiwa kupitia programu ya WhatsApp bila programu hiyo kuonyesha kama upo “online” au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo.
Kupitia makala hii nitaenda
kuonyesha njia mpya na rahisi ambayo unaweza kutumia ili kujibu meseji zako za
WhatsApp unazotumiwa bila programu ya WhatsApp kuonyesha kama upo online au
bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo yaani tiki mbili za blue.
Najua kila mtu anaweza kusema najua
hiyo lakini nakushauri endelea kusoma makala hii hadi mwisho kwani unaweza
kupata maujanja mapya ambayo pengine ulikuwa hujui kwa namna moja ama nyingine.
Kama kawaida sipendi kupoteza muda wako mwingi kwa maneno yangu, basi bila
kupoteza muda twende tukangalie njia ya kwanza.
Njia
ya Kwanza
Najua kuwa unaweza kusema kuwa
unaweza kuondoa last seen kwenye programu yako ya WhatsApp ili mtu asiweze
kujua kama umesoma meseji zake, lakini je unajua kuwa kuna njia nyingine rahisi
sana.? Kupitia simu yako hasa ya Android unaweza kusoma meseji za WhatsApp bila
programu hiyo kuonyesha kama upo online.
Unacho takiwa kufanya ni kusoma
meseji za WhatsApp kupitia sehemu ya Notification. Sehemu hii inapatikana juu
kabisa kwenye simu yako na hapo ndipo jumbe zote zinapo pitia kabla ya
kuonekana ndani ya programu husika. Unachotakiwa kufanya ni kuvuta sehemu hiyo
ya juu pale unapo pata ujumbe kisha bofya sehemu ya reply na kisha jibu ujumbe
huo ulio tumiwa. Kwa kufanya hivyo meseji itajibiwa bila kuonyesha kama upo
online.
Njia
ya Pili
Njia ya pili unahitaji kupakua
programu ya Unseen programu hii itakusaidia kusoma meseji za WhatsApp,
Instagram, Telegram na mitandao mingine mingi bila kuonekana “online”. Kama
wewe ni mmoja wa watu ambao wanapenda kusoma meseji za WhatsApp bila kuonekana
basi njia hii ni njia bora zaidi. Mbali na kuonekana online app hii pia
inasaidia kuzuia tiki mbili za blue ambazo huonyesha kuwa meseji imesomwa.
Unaweza kupata app hii kupitia PLAYSTORE AU APPSTORE na hakikisha kuwa una install na kutoa ruhusa zote kwenye app hiyo na moja kwa moja uta anza kusoma meseji za WhatsApp unazotumiwa bila mtu kujua kama umesoma meseji hizo.
KWAHERI KWA LEO
Comments
Post a Comment