Njia za Kutoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki (Njia
Rahisi)
Written by Stepado Pascal
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao
wanakuwa na tatizo la simu yako kustaki mara kwa mara basi makala hii ni kwa
ajili yako. Kama unavyojua, simu nyingi za Android za sasa zinakuja zikiwa
zimefungwa moja kwa moja na hauwezi kufunguka simu hiyo kwa namna yoyote.
Ni kweli kwamba njia rahisi ya
kuweza kuondoa simu kwenye hali ya kustaki ni kutoa battery ya simu hiyo na
kurudisha, lakini unafanyaje kama simu yako imefungwa moja kwa moja na huwezi
kufungua simu hiyo ili kutoa battery...? Majibu ninayo.
Kwanza awali ya yote labda nikwambie
kuwa, hatizo hili limenikuta binafsi na katika hali ya kufanya ufumbuzi nikaona
sio mbaya nikishiriki na wewe njia ambazo nilitumia kuweza kuondoa simu yangu
kwenye hali ya kustaki. Kumbuka njia hizi mara nyingi zinafanya kazi kwenye
simu za aina zote yaani simu za Android pamoja na simu za iPhone au iOS.Zipo njia nyingi sana lakin katika zote za haraka na rahisi kutumia ni hapa chini ,bhaas twende pamoja .....👇👇👇
- Chomeka Chaji

Kama simu yako imestaki na upo
karibu na chaji yake basi unaweza kuchukua hatua ya kwanza na kuchomeka simu
yako kwenye chaji ikiwa kwenye umeme. Kisha subiri kidogo na jaribu kuzima simu
yako. Njia hii hufanya kazi kwa simu nyingi ambazo unakuta zime staki kwa
sababu ya kufungua programu nyingi kwa wakati mmoja.
- Jipigie Simu
Njia nyingine ambayo unaweza kutumia
ni kupiga simu kwenye namba ambayo ipo kwenye simu iliyo staki. Mara nyingi
njia hii hufanya kazi hasa kama kuna programu uliyo kuwa unatumia ambayo ndio
imefanya simu yako kustaki. Njia hii kufanya kazi kwa sababu kupigiwa simu huwa
kuna fanya simu yako isimamishe kazi zote ikiwa pamoja na kusitisha Matumizi
yote ya data kwa muda.
- Shikilia Kitufe cha Home (Kama Kipo)
Kama simu yako ni ya muda kidogo,
bila shaka inayo kitufe cha home ambacho huwa tofauti na kioo cha simu yako.
Bofya kitufe hicho na kishikilie kwa utaratibu kwa muda wa sekunde tano na
utaweza kuona simu yako imetoka kwenye hali ya ku-staki. Njia hii inaweza
kufanya kazi kama simu yako inayo kitufe cha kujitegemea hivyo kama kitufe cha
home kipo kwenye kioo cha simu yako basi unaweza kujaribu njia inayofuata hapa
chini.
- Shikilia Vitufe vya Sauti + Kitufe cha Kuzima
Njia ambayo mara zote imekuwa
ikifanya kazi kwenye simu zote ambazo nimesikia zikiwa na tatizo la kustaki ni
njia hii ya kubonyeza kwa pamoja vitufe vyote vya sauti (kitufe cha kuongeza na
kupunguza sauti) ikiwa pamoja na kitufe cha kuzima na kuwasha simu. Bofya
vitufe vyote kwa pamoja kwa muda wa sekunde tano, au hadi utakapo ona simu yako
ikizima na kuwaka kwa mara nyingine. Njia hii ni moja kati ya njia ambayo
inafanya kazi kwenye simu nyingi sana hivyo unaweza kujaribu njia hii kama njia
zote hapo juu zimeshindikana.
Bila shaka hadi hapo umeweza kuondoa
simu yako kwenye hai ya kustaki, kama unataka kujua zaidi unaweza
kukomenti hapo chini .Ahsante tukutane tena wakati mwingine.....
Safi
ReplyDelete