Jinsi ya Kusoma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online Written by Stepado Pascal Ni wazi kuwa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia kuna sababu nyingi sana ambazo zinaweza kukufanya uwe na uhitaji wa kusoma meseji uliyotumiwa kupitia programu ya WhatsApp bila programu hiyo kuonyesha kama upo “online” au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo. Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia mpya na rahisi ambayo unaweza kutumia ili kujibu meseji zako za WhatsApp unazotumiwa bila programu ya WhatsApp kuonyesha kama upo online au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo yaani tiki mbili za blue. Najua kila mtu anaweza kusema najua hiyo lakini nakushauri endelea kusoma makala hii hadi mwisho kwani unaweza kupata maujanja mapya ambayo pengine ulikuwa hujui kwa namna moja ama nyingine. Kama kawaida sipendi kupoteza muda wako mwingi kwa maneno yangu, basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia ya kwanza. Njia ya Kwanza Najua kuwa unaweza kusema kuwa unaweza k...