Hizi Hapa Laptop 10 Bora za Kununua kwa Sasa (2020)
Written by Stepado Pascal
Ni mda mrefu sana umepita toka
tuongelee kuhusu laptop, pengine hii ni kutokana na uwepo wa laptop mpya chache
sana kwenye miaka ya karibuni au ni kwa sababu simu zimekuwa zikishika chati
zaidi kwa sasa pengine kuliko laptop, Lakini kama ulikua mmoja wa watu ambao
wanatamani kujua kuhusu laptop bora mwaka huu (2020) kabla haujaisha maana sasa
tupo jully na wewe ni kiu yako kumiliki laptop basi hii hapa ndio list ya
laptop bora ambazo unaweza kununua kwa sasa.
Kumbuka laptop hizi nyingi
zinapatikana hapa Tanzania hivyo tutajitahidi kuweka na bei za laptop hizi ili
uweze kujua angalau kwa makadirio ni kiasi gani cha fedha unachotakiwa kuwa
nacho ili uweze kupata aina flani ya laptop. Basi bila kupoteza muda twende
tuka angalie list hii, Kumbuka list hii haijapangwa kwa namba hivyo laptop zote
hapa ni bora sana kuwa nazo.
MacBook Pro Yenye Touch Bar
Ni wazi kuwa Macbook Pro yenye Touch
Bar ni laptop bora sana ya kununua kwa sasa, kama wewe ni mmoja ya watu ambao
wanafanya kazi za Ubunifu wa michoro mbalimbali (Graphics Design) basi hii ni
laptop muhimu na nzuri sana kwako. Bei ya Laptop Hii ni kuanzia Milioni Tsh
3,500,000 mpaka milioni Tsh 4,000,000.
Sifa
za MacBook Pro Yenye Touch Bar
- CPU:
Dual-core Intel Core i5 – i7
- Graphics:
Intel Iris Plus Graphics 640 – 650
- RAM: 8GB –
16GB
- Screen:
13.3-inch, (2,560 x 1,600) IPS
- Storage:
256GB – 1TB PCIe 3.0 SSD
Mazuri Kuhusu Laptop Hii
- Hii ndio Laptop bora kwa sasa kutoka Apple
- Processory ya Laptop hii inafanya kazi Haraka
Mabaya Kuhusu Laptop Hii
- Chaji yake Haidumu Sana
- Ni Bei Ghali Sana
Microsoft Surface Book 2 (13.5-inch)
Kama wewe ni mmoja ya watu ambao
wanapenda laptop inayoweza kubadilika na kuwa Tablet basi laptop hii
ya Microsoft Surface Book 2 (yenye inch 13.5) ni chaguo zuri sana kwako.
Mbali na uwezo wa laptop hii kuwa Tablet, laptop hii inauwezo mkubwa sana na ni
nzuri sana kwa wafanyakazi wa maofisini pamoja na wanafunzi. Bei ya Laptop hii
inaanzia Tsh Milioni 2,500,000 mpaka Tsh Milioni 3,500,000.
Sifa
za Microsoft Surface Book 2 (13.5-inch)
- CPU: Intel
Core i5-7300U – Intel Core i7-8650U 1.9GHz
- Graphics:
Intel UHD Graphics 620; Nvidia GeForce GTX 1050 (2GB GDDR5 VRAM)
- RAM: 8GB –
16GB
- Screen:
3,000 x 2,000 (267 ppi) PixelSense display, 3:2 aspect ratio
- Storage:
256GB – 1TB SSD
Kizuri Kuhusu Laptop Hii
- Battery Yake Inadumu na Chaji
- Laptop Hii ina nguvu Sana
Kibaya Kuhusu Laptop Hii
- Bei Ghali
- Haiji na Kalamu
Acer Switch 3
Kama wewe ni mpenzi wa laptop zenye
uwezo wa kubadilika na kuwa Tablet basi ni vyema ufahamu laptop hii, Laptop hii
ni moja kati ya laptop yenye nguvu zaidi na kizuri zaidi ni kuwa laptop hii
inapatikana kwa bei rahisi. Bei ya Laptop hii inaanzia Tsh 1,000,000 hadi Tsh
1,500,000.
Sifa
za Acer Switch 3
- CPU:
1.10GHz Intel Pentium Quad Core N4200 – Intel Core i3 7100U
- Graphics:
Intel HD Graphics 505
- RAM: 4GB
- Screen:
12.2-inch, 1920 x 1200 IPS LCD touchscreen
- Storage:
64GB – 128GB eMMC
Kizuri Kuhusu Laptop Hii
- Kwa Sura ni Nzuri Sanaa
- Bei Yake ni Rahisi
Kibaya Kuhusu Laptop Hii
- Sio Nzuri kwa Game
Apple MacBook 12-inch (2017)
Kama wewe ni mwanafunzi au
mfanyakazi ambaye unafanya kazi zako kwa kusafiri kila mara basi Apple
MacBook 12-inch (2017) ni laptop bora sana kwako, Mbali ya laptop hii kuwa na
uwezo mkubwa sana pamoja na kuwa nyepesi kuibeba, vilevile laptop hii ina uwezo
mkubwa sana wa kudumu na chaji hivyo inakupa uwezo wa kuendelea kufanya shughuli
zako za kila siku bila kuwa na wasi wasi wa kuisha chaji kwa haraka. Bei ya
laptop hii inaanzia Tsh 3,000,000 hadi Tsh 2,500,000
Sifa
za Apple MacBook 12-inch (2017)
- CPU: Intel
Core M3 1.2GHz – Intel Core i7 1.4GHz
- Graphics:
Intel HD Graphics 615
- RAM:
8GB – 16GB
- Screen:
12-inch, (2,304 x 1,440) IPS 16:10
- Storage:
256GB – 512GB SSD
Kizuri Kuhusu Laptop Hii
- Processor Yenye Nguvu Zaidi
- Battery Inadumu na Chaji Zaidi
Kibaya Kuhusu Laptop Hii
- Inayo Sehemu Moja ya USB-C port
- Ni Bei Ghali
Lenovo Yoga 920
Laptop hii pia ni moja kati ya
laptop zenye uwezo wa kubadilika na kuwa tablet, lakini utofauti wa laptop hii
ni kuwa, Laptop hii haitoki kama zilivyo laptop nyingine kwenye list hii,
Laptop hii yenyewe inazunguka nyuzi 360 na kukupa uwezo wa kufanya laptop hiyo
kuwa tablet. Kama wewe ni mwanafunzi au mfanyakazi wa ofisini laptop hii
itakufaa sana. Bei ya laptop hii inaanzia Tsh 4,500,000 hadi Tsh 3,500,000.
Sifa
za Lenovo Yoga 920
- CPU: Intel
Core i7-855OU
- Graphics:
Intel UHD Graphics 620
- RAM: 8GB –
16GB
- Screen:
13.9-inch 1920 x 1080 – 13.9-inch 3840 x 2160
- Storage:
256GB – 1TB SSD
- Connectivity:
802.11ac Wi-Fi; Bluetooth 4.1
- Camera:
720p front-facing
Kizuri Kuhusu Laptop Hii
- Inayo nguvu Sana ya Processor
- Ni nyembamba
Kibaya Kuhusu Laptop Hii
- Bei Ghali
- Haina Uwezo Mzuri wa Graphics
- Feni za Laptop Hii Zinatabia ya Kutoa Sauti
Asus Transformer Mini T102HA
Kama wewe unatafuta laptop ya bei
rahisi yenye uwezo wa kawaida basi laptop hii ni bora sana kwako, Laptop hii ni
nzuri sana kwa kufanya kazi ndogo ndogo za kila siku huku ikikupa uwezo wa kufungua
kurasa mbalimbali za tovuti pamoja na kazi zingine za kawaida. Bei ya Laptop
Hii ina anzia Tsh 1,000,000 mpaka Tsh 1,500,000.
Sifa
za Asus Transformer Mini T102HA
- CPU: Intel
Atom x5-Z8350
- Graphics:
Intel HD Graphics – Intel HD Graphics 400
- RAM: 2GB –
4GB
- Screen:
11.6-inch 1,366 x 768 HD IPS touchscreen
- Storage:
32GB
Kizuri Kuhusu Laptop Hii
- Laptop Hii ni Ndogo kwa Umbo na Nyepesi
- Inayo Uwezo Mkubwa wa Kudumu na Chaji
Kibaya Kuhusu Laptop Hii
- Haina Uwezo Mkubwa Sana
Asus Zenbook UX310UA
Kama wewe ni mtu unae hitajika
kufanya kazi kwa haraka kama vile mwandishi wa habari au watu walioko kwenye
kazi kama hizo, basi laptop hii ni bora sana kuwa nayo. Laptop hii inasifika
sana kwa tabia yake ya kuweza kuwaka kwa haraka na uwezo wake mzuri wa Processor.
Bei ya Laptop Hii ina anzia Tsh 2,000,000 hadi Tsh 2,500,000.
Sifa
za Asus Zenbook UX310UA
- CPU: Intel
Core i3 – i5
- Graphics:
Intel HD Graphics 620
- RAM: 8GB
- Screen:
13.3-inch up to QHD+ (3,200 x 1,800)
- Storage:
256GB SSD
Kizuri Kuhusu Laptop Hii
- Inauwezo wa Kuwaka na Kutumika Haraka
Kibaya Kuhusu Laptop Hii
- Battery Yake Haina Uwezo wa Kudumu Sana
Dell XPS 13
Hii ni moja kati ya laptop bora
sana, Kama wewe ni Mfanyakazi wa ofisi au mfanyakazi wa maswala ya ubunifu au
mtengenezaji wa Video laptop hii inauwezo wa kukuhudumia Vizuri, Laptop hii ni
moja kati ya laptop zenye nguvu na zinazo sifika kuwa laptop bora sana. Kama
ukituuliza Tanzania Tech ni laptop gani nzuri inayo tumia Windows ambayo
unaweza kununua ambayo itakusaidia hata kwa miaka ya mbeleni, basi Dell XPS 13
ni moja ya Laptop hizo ambazo tungekushauri kununua. Bei ya Laptop Hii ina
anzia Tsh 5,000,000 hadi Tsh 6,000,000.
Sifa
za Dell XPS 13
- CPU: 8th
generation Intel Core i5 – i7
- Graphics:
Intel UHD Graphics 620
- RAM: 8GB –
16GB
- Screen:
13.3-inch FHD (1,920 x 1,080) – 4k (3840 x 2160)
- Storage:
256GB – 1TB SSD
Kizuri Kuhsu Laptop Hii
- Inayo Uwezo wa 4K
- Uwezo Mzuri wa Gharphics (Japo Sio Sana)
Kibaya Kuhusu Laptop Hii
- Bei Ghali Sana
Lenovo Yoga Book
Kama wewe unatafuta laptop ya bei nafuu
na yenye uwezo wa tofauti kidogo basi Laptop Hii ni moja kati ya laptop
zitakazo kufaa sana. Laptop hii inauwezo mzuri sana wa kioo pamoja na uwezo
wake wa kubebeka kirahisi kutokana na uzito wake mdogo. Bei ya Laptop Hii
Inaanzia Tsh 800,000 hadi Tsh 1,000,000.
Sifa
za Lenovo Yoga Book
- CPU: Intel
Atom x5-Z8550
- Graphics:
Intel Atom
- RAM: 4GB
- Screen:
10.1-inch full HD IPS touchscreen
- Storage:
64GB SSD, up to 128GB microSD
Kizuri Kuhusu Laptop Hii
- Laptop Hii ni Nyepesi na Nyembamba
- Kioo Kizuri
- Bei Rahisi
Kibaya Kuhusu Laptop Hii
- Inatumia Processor Yenye Uwezo Mdogo
Dell XPS 15
Sasa hapa naomba niwe wazi, Laptop
hii ni moja kati ya laptop ninayo ipenda sana na kuitamani sana kuwa nayo,
hivyo basi inawezekana mapenzi yangu ni moja kati ya sababu ya laptop hii
kuwepo hapa. Pamoja na hayo nikisema laptop bora basi hii ni moja kati ya
laptop bora sana na yenye uwezo mzuri sana. Kwa mujibu wa tovuti ya Techradar
Hii ndio laptop bora kutoka Dell Mpaka Sasa. Bei ya Laptop Hii ina anzia Tsh
2,500,000 hadi Tsh 3,500,000.
Sifa
za Dell XPS 15
- CPU: Intel
Core i5-7300HQ – i7-7700HQ
- Graphics:
NVIDIA® GeForce GTX 1050 with 4GB GDDR5
- RAM: 8GB –
16GB DDR4
- Screen:
Up to 15.6-inch Ultra HD (3840 x 2160) InfinityEdge touchscreen
- Storage:
1TB HDD – 512GB SSD
Kizuri Kuhusu Laptop Hii
- Inadumu na Chaji
- Kioo Bora
- Uwezo Mzuri wa Processor
Kibaya Kuhusu Laptop Hii
- Kamera Yake (Web Cam) Imekaa Mahali Pabaya
Na hiyo ndio list ya Laptop bora ambazo unaweza kununua kwa sasa na vilevile hizi ndio laptop bora mpaka sasa mwaka huu 2019 – 2020.Tukutane tena wakati mwingine..
Comments
Post a Comment