Mambo Muhimu Kama Unataka Kufanikiwa Biashara Mtandaoni Imeandikwa na Stepado Pascal Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanafikiria kuanza biashara yoyote mtandaoni basi nakukaribisha kwenye makala hii, Kupitia makala hii nitakwambia mambo ambayo unatakiwa kujua kabla ya kuanza biashara hiyo ikiwa pamoja na njia za muhimu za kufuata ili kufanikiwa. Kabla ya yote ni vyema niwe mkweli, mimi binafsi yangu bado sijafanikiwa kwa asilimia 100, ila pia siwezi kusema kuwa sijawahi kuona mafanikio ya biashara mtandaoni, hivyo nadhani kwa ujuzi wangu huo mdogo ninaweza kukupa mambo mawili matatu ambayo yamenisaidia mimi kuwa na mafanikio hayo madogo. Basi baada ya kusema hayo, moja kwa moja twende kwenye makala hii ya leo. Subira ni Muhimu Sana Kama wewe ulishawahi kufanya biashara yoyote basi lazima unajua kuwa biashara yoyote inahitaji subira. Hii ni muhimu sana kuliko mambo yote kwani unaweza kuwa na furaha wakat...