Jinsi ya Kutumia Mtandao wa TikTok Hatua kwa Hatua
Written Stepado Pascal
Kutokana na kuwa mtandao huo umekuwa ni maarufu na kutumiwa na watu wengi sana, leo nimeona nikuandalie makala fupi na rahisi ambayo itakusaidia kujua jinsi ya kutumia mtandao wa TikTok pamoja na kufahamu kazi ya vitu mbalimbali ndani ya app hiyo. Basi bila kuendelea kupoteza muda wako zaidi twende moja kwa moja kwenye makala hii.
Muonekano wa Mtandao wa TikTok
Mara baada ya kupakua app ya TikTok, utaweza kupata muonekano ambao ni
mrahisi kwa watumiaji wa muda mrefu, lakini kama wewe ni mgeni na hii ndio mara
yako ya kwanza kutumia mtandao wa TikTok basi hivi ndivyo mtandao huo unavyo
onekana kwenye ukurasa wa mwanzo.Kama unavyoweza kuona hapo juu utakapo ingia kwanza kwenye mtandao wa TikTok sehemu za muhimu kwa sasa ni sehemu hizo tatu ambazo nime kuonyesha. Sehemu hizo hutumiwa na watu wengi hasa wale ambao ni wageni kwenye app hiyo. Kwa ufupi kabisa hizi ndio kazi za sehemu hizo tatu ambazo nime kuonyesha hapo juu.
- Sehemu hii
hutumika zaidi kufuata watu au kuangalia video ambazo zinaendana na wewe,
naposema zina endana na wewe hapa nina maana kuwa, mtandao wa TikTok
unatumia mfumo wa AI ambapo kadri unapo angalia video ndivyo inapojua
zaidi video unazo zipenda na ndivyo unavyo endelea kuziona zaidi kwenye
ukurasa huo.
- Kupitia
sehemu ya pili hapo juu utaweza kutumia sehemu hiyo kuangalia profile ya
mwenye video, chini yake ni sehemu ya kulike video hiyo, na chini yake ni
sehemu ya kutoa maoni, na kama simu yako inayo kioo kifupi utaweza kuona
vidoti vitatu ambavyo ukigusa hapo utaona alama ya mshale ambayo
itakuruhusu kushare video hiyo kwenye mitandao mingine au kudownload,
pamoja na mambo mengine.
- Sehemu ya
mwisho hii itakusaidia kuona video nyingine ambazo zimetumia sauti ambayo
video hiyo imetumia. Hapa utaweza kuona video nyingi tofauti zenye sauti
hiyo hiyo iambayo inafanana na kwenye video unayo angalia kwa wakati huo.
Sehemu hii ni muhimu na ndio yenye kuleta utofauti wa mtandao wa TikTok na
mitandao mingine.
Jinsi ya Kupost
Video Kwenye Mtandao wa TikTok
Baada ya kujua kuhusu sehemu hizo za muhimu sasa endelea kwenye hatua ya
pili ambapo ni jinsi ya kupost video kwenye mtandao wa TikTok. Kupitia hapa
utaweza kupost video za kuweka au ku-upload, au unaweza kutengeneza video zako
kwa kurekodi kupitia app ya TikTok, utaweza kurekodi video zenye urefu wa
sekunde 15 hadi sekunde 60.Ili kurekodi fungua sehemu hiyo kisha bofya kwa kushikilia kitufe chekundu kilichopo chini mwisho wa kioo cha simu yako, angalia kwa juu utaweza kuona mstari wenye kuonyesha muda wa video, hii itakusaidia sana ili kujua pale sekunde 15 au 60 zinapofikia mwisho.
Effect za TikTok
Wakati unarekodi upande wa kulia utaweza kuona sehemu mbalimbali ambazo zinaweza kukusaidia kufanya mambo mbalimbali, sehemu ya kwanza juu itakusaidia kubadilisha kamera ya mbele na nyuma. sehemu inayofuata itakupa uwezo wa kuongeza speed ya video, sehemu inayofuata utaweza kuweka filter mbaimbali na sehemu inayofuata itakupa effect ya Beautify na sehemu ya mwisho ni sehemu ya kuweka Timer ambayo najua kila mtu anafahamu.
Kuweka Sauti
au Sound kwenye Video zako za TikTok
Kabla ya kurekodi video yako kama unataka kurekodi video ambayo wewe unaimba
nyimbo za wanamuziki maarufu basi unaweza kutumia sehemu ya Sound kuweza kuweka
sehemu ya nyimbo ya msanii unaemtaka. Unaweza kubofya sehemu ya Sound iliyopo
juu mwanzo kwenye app ya TikTok.Baada ya kubofya hapo utaweza kuletewa ukurasa ambao unaweza kutumia kutafuta nyimbo unayotaka, au unaweza kutumia nyimbo yoyote ambayo ina trendy kwa muda huo au kwa maneno mengine kama nyimbo imetumika sana ndani ya app hiyo na watu wa Tanzania basi utaweza kuiona hapo juu pale unapo fungua ukurasa huo.
Baada ya hapo unaweza kuchagua nyimbo unayopenda kisha anza kurekodi na utaweza kuona nyimbo inaimba kila utakapokuwa unabofya na kushilia kitufe cha kurekodi. Baada ya hapo sasa unaweza kuendelea kwa kuchagua sehemu ya maneno yaani description kisha chagua hashtag kwani hizi ni muhimu sana kwenye mtandao wa TikTok, baada ya hapo sasa post video yako.
Kurekodi video zenye
Sauti za Watu Wengine
Kama unataka kurekodi video ambazo zinakuja na sauti za watu wengi, unaweza
kufuata hatua hizi fupi. Hatua ya muhimu unapokua una angalia video yenye
maneno ambayo umeyapenda moja kwa moja bofya kufe kilichopo chini upande wa
kulia kwenye kona, kitufe hicho kinaonekana na kinazunguka na kutoa alama za
muziki.Bofya hapo kisha bofya use this sound, na moja kwa moja anza kurekodi kwa kushikilia kitufe cha katikati chekundu na utaweza kuona sauti hiyo inaongea nyuma ya video yako wakati ukiwa unarekodi. Baada ya hapo unaweza kupost video yako moja kwa moja.
Hadi hapo natumaini utakuwa umeweza kutumia mtandao wa TikTok kwa urahisi kabisa, kama kunayo sehemu yoyote ambayo utakuwa umekwama basi unaweza kutuandikia kupitia sehemu ya maoni hapo chini.
SHUKRANI TUKUTANE WAKATI MWINGINE
Comments
Post a Comment