Je Kuwa na Subscriber Wengi Ndio Kupata Pesa Nyingi YouTube
Written by Stepado Pascal
3-4 minutes
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao
wana miliki akaunti kwenye mtandao wa youtube basi pengine hii ni sababu ya
wewe kusoma makala hii, kama huna akaunti kwenye mtandao wa youtube na ulikuwa
unafikiria kuwa na akaunti basi pengine ni vizuri kusoma makala hii kabla ya
kuendelea kwenye hatua ya kufungua channel yako.
Kupitia makala hii nitaenda
kukwambia ni njia gani za kutumia kupata pesa zaidi kwenye mtandao wa youtube
ikiwa pamoja na kujibu baadhi ya maswali ambayo pengine yalikua yanakusumbua
sana.
Kwa kuanza labda tukubaliane kwamba, Subscriber ni sehemu muhimu sana kwenye channel
yako hasa kama unatarajia kuanza au ndio kwanza umeanza. Pia ukumbuke kuwa
subscriber ndio kitu cha muhimu kinacho saidi wewe kuanza kutengeneza pesa
kwenye channel yako kutokana na sheria ya youtube ambayo ina ainisha kuwa na
subscriber pamoja na views kuanza kutengeneza pesa kupitia mtandao wa YouTube.
Kama unavyoweza kuona, kwa mujibu wa
youtube unahitaji kuwa na subscriber wasio pungua 1000 na views 4000 ndani ya
kipindi cha mwaka mmoja au miezi 12. Hii tu ni sehemu ambayo inaonyesha kuwa
subscribers ni muhimu sana tena zaidi kama unataka kuanza. Hivyo basi, wakati
unafikiria kuanzisha channel kwaajili ya kujipatia kipato mtandaoni ni muhimu
kuangalia subscriber ili kufikia malengo yako mapema.
Je
Subscribers Wengi Ndio Pesa Nyingi Youtube.?
Jibu la moja kwa moja kwenye swali
hilo ni HAPANA, kuwa na subscriber wengi haku maanishi kuwa channel fulani
inaingiza kipata kwa wingi au lah. Bali hii ufikiriwa hivyo kwani watu wengi
hudhania kuwa na subscriber wengi ndio hufanya watu wengi zaidi kuangalia video
hivyo mtu kutengeneza kipato zaidi.
Je
Kitu Gani Kinaweza Kusaidia Kutengeneza Pesa Zaidi YouTube.?
Jibu la moja kwa moja la swali hili
ni VIEWS, haijalishi una subscribers wangapi kwenye channel yako kitu cha
muhimu ni views. Watu wengi wanapo angalia video zako hii ina maanisha kuwa
watu wengi wanaona matangazo yanayopita kwenye video zako hivyo kutengeneza
pesa zaidi, hii ni muhimu kwani mtu anaweza kuona video zako bila hata kuwa
mmoja wa subscribers wako. Hivyo ni muhimu kutengeneza Views nyingi zaidi kama
unataka kutengeneza pesa zaidi.
Je
Unawezaje Kujua Kama Channel Inatengeneza Pesa Zaidi.?
Kama unataka kujua kama channel
inatengeneza pesa nyingi zaidi basi unaweza kuangalia jumla ya views ambayo
inapatikana kwenye ukurasa wa about kwenye channel yako au ya mtu yoyote.
![]() |
kama inavyo onekana hapa views wa channeli ya youtube |
Kama unavyoweza kuona hiyo ni idadi
ya views, views hizo ndio zinaweza kuonyesha kiasi cha pesa ambacho channel
inaweza kutengeneza, unaweza kurekodi kwa wiki views zilikuwa ngapi alafu baada
ya wiki unaweza kuangalia kujua kama views zimebadilika kwa kiasi kikubwa. Kama
kuna mabadiliko makubwa basi channel hiyo inatengeneza pesa nyingi zaidi.
Je
Unafanyaje Kuongeza Views Zaidi.?
Ukweli ni kwamba hata mpaka sasa
binafsi najifunza kuongeza view kwenye video zetu, lakini kifupi ni kuwa hakuna
njia moja ya kuongeza view kwenye video, zipo njia nyingi sana za kuongeza view
ikiwa pamoja na kushare video kwenye mitandao ya kijamii na mengine mengi ya
muhimu. Unaweza kufanya mambo haya machache ili kuongeza views.
ü Andika vichwa vya habari vinavyo vutia watu zaidi.
ü Weka Thumbnail au picha za video zinazo vutia zaidi.
ü Tengeneza video zenye ubora.
ü Tengeneza video zenye kutoa elimu ambayo itasaidia video
zako kuangaiwa zaidi.
ü Tengeneza video zinazodumu YouTube.
ü Shiriki video kwenye mitandao yako ya kijamii.
ü Tumia sehemu ya Discussion kutangaza video zako.
Mpaka hapo natumaini umejua kuwa
views ni muhimu kuliko subscriber kwenye channel yako. Kumbuka ni muhimu kuweka
video mpya mara kwa mara kwani hii itasaidia watu kuweza kujua channel yako na
kutazamwa zaidi na hivyo kutengeneza pesa Zaidi,pia ni muhimu kuweka time table
ya jinsi unavo post video katika channel yako kwani itakusaidia kuwa na watu
wengi Zaidi.
stepado.blogspot.com tumejikita
kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi wakati
wote. Nawapenda sana
Comments
Post a Comment