Skip to main content

Mambo Muhimu Kama Unataka Kufanikiwa Biashara Mtandaoni.


Mambo Muhimu Kama Unataka Kufanikiwa Biashara Mtandaoni

Imeandikwa na Stepado Pascal

                Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanafikiria kuanza biashara yoyote mtandaoni basi nakukaribisha kwenye makala hii, Kupitia makala hii nitakwambia mambo ambayo unatakiwa kujua kabla ya kuanza biashara hiyo ikiwa pamoja na njia za muhimu za kufuata ili kufanikiwa.
Kabla ya yote ni vyema niwe mkweli, mimi binafsi yangu bado sijafanikiwa kwa asilimia 100, ila pia siwezi kusema kuwa sijawahi kuona mafanikio ya biashara mtandaoni, hivyo nadhani kwa ujuzi wangu huo mdogo ninaweza kukupa mambo mawili matatu ambayo yamenisaidia mimi kuwa na mafanikio hayo madogo. Basi baada ya kusema hayo, moja kwa moja twende kwenye makala hii ya leo.

Subira ni Muhimu Sana



Kama wewe ulishawahi kufanya biashara yoyote basi lazima unajua kuwa biashara yoyote inahitaji subira. Hii ni muhimu sana kuliko mambo yote kwani unaweza kuwa na furaha wakati unaanza biashara yako siku za kwanza, lakini pale unapo ona siku zinaenda na hujapata mteja yoyote basi unakata tamaa au una punguza nguvu.
Kwenye biashara mtandaoni pia unahitaji subira zaidi kuliko kitu chochote, kwani wakati unatengeneza website yako ya kwanza usitegemee kupata watumiaji wengi kwa mara moja bali jiandae kisaikolojia kuwa na moyo wa subira kwani hili huwa linachukua muda hasa kama huna pesa ya kufanya promotion.

Usipende Shortcut



Kuna watu wengi sana siku hizi kufanya biashara mtandaoni ambazo hutegemea watu wengine kwa asilimia 100. Hii ni pale ambapo unakuta mtu anae tengeneza website ambayo inachukua makala au habari kutoka kwenye tovuti nyingine na mtu huyo hufanya kama vile makala hizo ni za kwake au amechapisha yeye. Mara nyingi biashara za namna hii huwa hazifanikiwi.
Kwa mujibu wa Google, biashara za mtandaoni siku hizi hutegemea zaidi brand kuliko hata makala au habari ambazo mtu anaweka kwenye tovuti yake. Hivi karibuni Google imeleta kitu kinaitwa E-A-T. Maneno hayo husimama badala ya maneno (Expertise, Authoritativeness, and Trustworthiness), hii ni njia ambayo Google hutumia kuangalia website zenye habari au makala ambazo zime andaliwa na wataalamu wa sekta hiyo.
Kwa mfano kama wewe ni dokta na unayo tovuti ya makala za afya, basi ni rahisi sana kufanikiwa kwenye biashara mtandaoni, pia vilevile kama tovuti yako ipo mtandaoni siku nyingi na imejikita kwenye upande fulani maalum kwa muda mrefu basi ni rahisi biashara yako kufanikiwa. Google imetangaza kuwa kama tovuti haijatengeneza brand yake yenyewe ni ngumu kufanikiwa mtandaoni.

Fanya Biashara Inayotatua Matatizo ya Watu



Kuna utofauti mdogo sana kati ya biashara bora na biashara unayopenda. Hii ni sawa na kukwambia kuwa hakikisha unafanya biashara unayopenda, lakini pia hakikisha biashara hiyo inatatua matatizo ya watu au jamii iliyo kuzunguka. Mara nyingi kama unataka kufanya biashara mtandaoni ni vizuri kuangalia changamoto ambazo wewe mwenyewe binafsi unazipata.
Hii ni sawa na kusema kuwa, wazo bora la biashara mtandaoni linatoka kwenye maisha yako ya kila siku. Kama unaona kuna uhitaji wa kuanzisha tovuti inayohusu ufugaji kwa sababu unaona ukitafuta kitu kuhusu ufugaji mtandaoni hupati kitu unacho kitaka basi go for it.. hilo litakuwa wazo bora.

Usiangalie Pesa Kwanza



Point zote hizo hapo juu zinakuja kwenye point hii, Ni muhimu sana kutoweka pesa mbele kwani biashara yoyote ambayo inaweka pesa mbele huwa haina mafanikio ya muda mrefu. Nadhani wote tunakumbuka kuwa Facebook ilianza kutumika bila matangazo na ilitumika hivyo kwa muda mrefu sana zaidi ya miaka 2.
Baadae ndipo Facebook ilianza kuleta matangazo kidogo kidogo hadi sasa unaona kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kumiliki biashara kubwa mtandao kama Instagram, WhatsApp na nyingine nyingi ambazo hazijulikani. Hapa ndio ambapo unatakiwa kujumuisha point zote hapo juu kwenye sentensi moja ambayo itasomeka hivi “kuwa na subira, usipenda shortcut na hakikisha una tatua matatizo ya watu kabla ya kuwaka pesa mbele”.

Nenda Sambamba na Mabadiliko



Baada ya kufanya yote hayo hapo juu, basi hatua ya muhimu ya mwisho ni kuhakikisha unaenda sambamba na mabadiliko. Ni muhimu kujua kuwa internet inabadilika na kadri siku zinavyo kwenda mambo mengi yanazidi kupitwa na wakati na mengine yanazidi kuja kwa kasi.
Kwa mfano siku hizi unaona mtandao wa TikTok umeanza kuwa maarufu na hii inafanya Facebook na mitandao mingine kufikiria kuja na teknolojia zinazo fanana na TikTok hivyo pengine tegemea hivi karibuni kuona mengi yanayo fanana na mtandao wa TikTok kwenye mitandao mingine kama Instagram pamoja na Facebook pengine hata WhatsApp.
Ni muhimu kuendana na teknolojia pamoja na wakati kama unataka kufanya biashara yoyote mtandaoni, hivyo ni muhimu kuwa na ujuzi wa kuweza kutengeneza tovuti au biashara ambayo utaweza kuisimamia na kuendeleza hasa kwenye upande wa teknolojia.

Hitimisho

Na hayo ndio mambo ya muhimu ambayo unatakiwa kujua pale unapotaka kuanzisha biashara yoyote mtandaoni, kumbuka ni muhimu kujua kuhakikisha unafuata mambo yote haya na hapo na kuhakikishia utakuwa umepiga hatua kuelekea kwenye mafanikio ya biashara mtandaoni.



Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kusoma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online

  Jinsi ya Kusoma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online Written by Stepado Pascal Ni wazi kuwa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia kuna sababu nyingi sana ambazo zinaweza kukufanya uwe na uhitaji wa kusoma meseji uliyotumiwa kupitia programu ya WhatsApp bila programu hiyo kuonyesha kama upo “online” au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo. Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia mpya na rahisi ambayo unaweza kutumia ili kujibu meseji zako za WhatsApp unazotumiwa bila programu ya WhatsApp kuonyesha kama upo online au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo yaani tiki mbili za blue. Najua kila mtu anaweza kusema najua hiyo lakini nakushauri endelea kusoma makala hii hadi mwisho kwani unaweza kupata maujanja mapya ambayo pengine ulikuwa hujui kwa namna moja ama nyingine. Kama kawaida sipendi kupoteza muda wako mwingi kwa maneno yangu, basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia ya kwanza. Njia ya Kwanza Najua kuwa unaweza kusema kuwa unaweza k...

Download Programu ya Microsoft Office 2019 Pro Plus

Download Programu ya Microsoft Office 2019 Pro Plus Written by STepado pascal Ikiwa tunazungumzia programu bora kwaajili ya ofisi ni wazi kuwa programu ya Microsoft Office ni programu bora sana kwako, programu hii inakuja na uwezo mkubwa sana wa kusaidia mtu ambaye anafanya kazi kwenye ofisi, au hata kama wewe ni mwanafunzi programu hii ni bora sana kwako. Kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia sana kuweza kupata programu ya Microsoft Office 2019 Pro Plus, ambayo imesheheni sifa nyingi sana bure bila kulipia gharama yoyote. Kumbuka hili ni toleo la Pro Plus hivyo limesheheni sifa zote za programu ya Microsoft Office. Baadhi ya programu ambazo zipo ndani ya toleo hili ni pamoja na –     Microsoft Word     Microsoft Excel     Microsoft Powerpoint     Microsoft Outlook     OneNote     OneDrive     Microsoft Teams Kwa kuanza ni vyema kufahamu kuwa programu hii ni kwa ajili ya kompyuta za Windows na inafany...

Kuanzia A-Z List zote za Windows CMD Commands

A-Z List 0f Windows CMD Commands  By  Am IT guy STEPADO Zifuatazo ndizo   list zote za Windows CMD commands  ambazo nimezipangilia katika alphabetically CMD commands. Command Prompt  and  CMD Commands  are unknown territories for most of the Windows users, they only know it as a black screen for troubleshooting the system with some fancy commands. repair a corrupted disk, hide certain drives, to create a hacking-like environment, etc. Nini maana ya Command Prompt na CMD Commands? Command Prompt, kwa jina jingine ni  cmd.exe  or  cmd  —   ni  command line amabyo inatumika kutafsiri application  katikaWindows NT family operating systems. Na CMD Commands ni specific set of instructions given to Command Prompt to perform some kind of task or function on your Windows PC. Most of the Windows CMD Commands are used to automate tasks via script  and batch files, perform advanced administrative functi...

Jinsi ya Ku-install Windows 10, 8, 7 na XP Kwenye Simu za Android

 Jinsi ya Ku-install Windows 10, 8, 7 na XP Kwenye Simu za Android Written by STepado Pascal windows kwenye android (1) Kutokana na teknolojia kubadilika sana vile vile hata simu zetu nazo zimekua zikibadilika kila siku, simu zetu zimekuwa zimebadilika kuanzia uwezo, vitu inavyofanya mpaka matumizi ya simu hizo. kuelewa mabadiliko hayo leo Tanzania Tech tunaenda kukuonyesha njia rahisi ya kuinstall Windows 7, Windows 8, Windows 10 pamoja na Windows XP kwenye simu yako ya Android. Kwa kuanza ni vyema ukajua kuwa uwezo wa kutumia Windows kwenye simu yako unaweza kukusaidia wewe kutumia simu yako kama kompyuta, njia hii itakusaidia sana kama simu yako inauwezo wa kutumika kwenye screen kubwa ili kukupa uwezo wa kufanya vitu mbalimbali kama unavyo tumia kwenye kompyuta, yaani bila tofauti kubwa utafauti ni kwenye graphics pekee. Kwa kuanza unatakiwa kuwa na simu yako ya Android yenye RAM at-list GB 1 na kuendelea, uharaka wa kuinstall Windows kwenye simu yako unategemeana sana na Uwezo...

Njia za Kutoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki (Njia Rahisi)

Njia za Kutoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki (Njia Rahisi) Written by Stepado Pascal Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanakuwa na tatizo la simu yako kustaki mara kwa mara basi makala hii ni kwa ajili yako. Kama unavyojua, simu nyingi za Android za sasa zinakuja zikiwa zimefungwa moja kwa moja na hauwezi kufunguka simu hiyo kwa namna yoyote. Ni kweli kwamba njia rahisi ya kuweza kuondoa simu kwenye hali ya kustaki ni kutoa battery ya simu hiyo na kurudisha, lakini unafanyaje kama simu yako imefungwa moja kwa moja na huwezi kufungua simu hiyo ili kutoa battery...? Majibu ninayo. Kwanza awali ya yote labda nikwambie kuwa, hatizo hili limenikuta binafsi na katika hali ya kufanya ufumbuzi nikaona sio mbaya nikishiriki na wewe njia ambazo nilitumia kuweza kuondoa simu yangu kwenye hali ya kustaki. Kumbuka njia hizi mara nyingi zinafanya kazi kwenye simu za aina zote yaani simu za Android pamoja na simu za iPhone au iOS.Zipo njia nyingi sana lakin katika zote...

Link ya kupata windows

Mambo vp Wana blog ,leo nimekuletea link hii hapa chini ,uweze kupakuwa window yoyote uitakayo kwa matumizi yako ,hvo basi bila kupoteza wakati click hiyo link hapo itakupeleka kupakuwa windows. Ukipata changamoto yoyote niachie comments yako hapo chini au chochote Cha kushare nasi karibu Sana.Tukutane tena wakati mwingine Click hapa

Antivirus ipi Bora zaidi kwa Windows 10?

Welcome in Technology   MAADA LEO *Anti-virus Ipi ni Bora zaidi kwa Windows 10?*  *By Am IT guy STEPADO* Windows 10 haitaingilia kazi mara kwa mara kukutaarifu kupakia ‘Anti-virus’ kwenye mashine yako kama vile Windows 7 ilivyokuwa ikifanya. Hii ni kwa sababu kuanzia Windows 8, Microsoft walifanya uamuzi wa msingi wa kuweka Anti-virus moja-kwa-moja kwenye mfumo wao. Antivirus hii inaitwa Windows Defender na ni Antivirus ambayo Microsoft wenyewe wanaitoa bure pamoja na WIndows mpya. Kwa maana hiyo swali la msingi la makala hii linafaa kubadilika na kuwa – ‘Je Windows Defender ni antivurus ni bora zaidi kwa usalama wa kompyuta yako au la?’ Windows Defender WIndows Defender inatokana na Microsoft Security Essentials (MSE) na ni, kwa maneno mengine, toleo la kisasa zaidi la MSE, ambayo ilikuwa ni antivirus ya bure kabisa kwa ajili ya Windows 7. Kwa sasa, antivirus ya Windows Defender inakuja pamoja na Windows na ni ngome ya kwanza kwa kompyuta yako. *Je, Windows Defender Inatosha...