Skip to main content

Tofauti ya Processor za Mediatek Helio na Qualcomm Snapdragon

Tofauti ya Processor za Mediatek Helio na Qualcomm Snapdragon
Written by Stepado Pascal

Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanatumia smartphone au umekuwa msomaji watu hapa Stepado.blogspot.com basi lazima umesha sikia tukisema sana kuhusu processor za Mediatek na Snapdragon. Sasa kutokana na mijadala mbalimbali mitandaoni kuhusu processor hizi mbili leo nimeona nikuletee makala fupi yenye kuonyesha tofauti kati ya processor za Mediatek na Snapdragon.
Kupitia makala hii sitoingia ndani sana na kuanza kuzungumza historia ya kampuni hizi mbili bali nitatumia muda huu kukwambia vitu vya muhimu ambavyo nadhani vinaweza kufanya uweze kuona tofauti kati ya processor hizo mbili. Basi bila kupoteza muda twende tukangalie tofauti hizi.
Utengenezaji


Kwa kuanza labda tuongelee tofauti ya utengenezaji wa processor za Mediatek Helio na Qualcomm Snapdragon. Kwa upande huu kampuni zote mbili hazitengenezi processor zake zenyewe bali kampuni hizi mbili zote hufanya ubunifu wa mitindo ya processor ikiwa pamoja na kufanya tafiti mbalimbali na baadae processor hizo hutengenezwa na kampuni inayoitwa ARM Holdings.
Tofauti kubwa kwenye upande wa utengenezaji wa Processor hizi ni upande wa GPU, Mediatek hutumia GPU za Mali ambazo hizi pia utengenezwa na ARM Holdings, lakini kwa upande wa Snapdragon wao hutumia GPU za Adreno ambazo hizi hutengenezwa na Qualcomm wenyewe.
Hivyo basi, utaweza kuona tofauti ya utengenezaji wa processor za Mediatek Helio na Qualcomm Snapdragon ni kuwa GPU za Snapdragon hutengenezwa na Qualcomm wenyewe wakati GPU za Mediatek hutengenezwa na ARM na ndio maana mara nyingi GPU hizi huitwa ARM Mali (GPU).
Uwezo wa GPU

Kutokana na Qualcomm kutengeneza GPU zake yenyewe mara nyingi GPU za Qualcomm ambazo ni Adreno huwa na uwezo mzuri zaidi tofauti na GPU za Mali ambazo hutumiwa kwenye processor za Mediatek. Hii inaweza kuonekana kwenye baadhi ya simu hasa kwa wale wapenzi wa Game wanaweza wakawa wanajua zaidi kuhusu hili, mara nyingi simu zenye GPU za Mali huwa na matatizo ya kupata moto sana tofauti na GPU za Adreno hasa unapokuwa unacheza game zenye uwezo mkubwa.
Lakini pamoja na hayo GPU za Mali huwa na uwezo mkubwa wa speed tofauti na GPU za Adreno ndio maana mara nyingi simu zenye GPU za Mali hupata joto kutokana na kutumia kiasi kikubwa cha chaji kuendesha GPU yenyewe unapokuwa unacheza game, ukilinganisha na GPU za Adreno kutoka Qualcomm Snapdragon ambazo hutumia kiasi kidogo cha chaji kuendesha GPU zake.
Uwezo wa CPU

Kwa upande wa uwezo wa CPU mpaka sasa najua unajua kuwa kampuni zote hzitengenezi processor zake zenyewe isipokuwa GPU za Adreno zenyewe hutengenezwa na kampuni ya Qualcomm yenyewe.
Lakini pamoja na hayo kampuni ya Qualcomm yenyewe baada ya kupokea processor zake kutoka kwa kampuni ya ARM Holdings hufanyia mabadilIko na maboresho ya CPU na kuziongezea uwezo zaidi na kutengeneza processor zake zenye ubora zaidi kama vile Kryo CPU ambazo hizi ni sawa na kusema ni CPU zilezile lakini zimeongezewa uwezo zaidi na kampuni ya Qualcomm.
Kwa upande wa Mediatek yenyewe huchukua processor hizo na kuzitumia kama zilivyo hivyo utaweza kuona kuwa processor za Qualcomm Snapdragon zinaweza kufanya kazi vizuri zaidi kwenye upande wa CPU, tofauti na processor za Mediatek ambazo hutumika kama zilivyo kutoka kampuni ya ARM Holdings.
Gharama
Sasa kutokana na kampuni ya Qualcomm kubadilisha kidogo processor zake hii upelekea processor za Qualcomm Snapdragon kuwa za gharama zaidi kuliko zile za Mediatek na unaweza kuona hili kwenye simu nyingi zenye processor za Qualcomm Snapdragon.
Mara nyingi simu zenye processor hizo huwa zinapatikana kwa bei ghali zaidi kuliko simu zenye processor za Mediatek, hii inatokana na gharama za zaidi ambazo kampuni ya Qualcomm huingia kutengeneza processor hizo za Snapdragon hasa kwenye upande wa CPU.
Utumiaji
Sasa baada ya kuongelea hayo hebu tuongelee kidogo kuhusu utumiaji, Mara nyingi simu zenye processor za Mediatek huchelewa sana kupata matoleo mapya ya mifumo ya uendeshaji tofauti na simu zenye processor za Snapdragon.
Hii hutokana na mfumo mzima unaotumiwa na Mediatek sio mifumo huru (Open Source) hivyo ni ngumu kwa wabunifu wa programu kuweza kupata nafasi ya kutengeneza kwa haraka mifumo ya uendeshaji kwaajili ya simu zenye processor hizo. Lakini kwa upande wa Snapdragon hakuna matatizo yoyote ya simu zenye processor hizo kuchelewa kupata matoleo mapya ya mfumo wa uendeshaji.
Battery
Pia vile vile kwa sababu nilizo kwambia hapo awali, Mara nyingi simu zenye processor za Mediatek hutumia chaji zaidi ya simu zenye processor za Qualcomm Snapdragon hii hutokana na kuwa processor hizi hutumia Core nyingi zaidi kwenye chipset zake hivyo hutumia chaji zaidi kuweza kuendesha processor hizo.
Pia kwa upande wa GPU kama nilivyo kwambia awali simu zenye processor za Mediatek hutumia GPU zenye Speed zaidi hivyo speed kubwa ni lazima iende sawa sawa na uwezo wa battery. “More speed more battery”.
Hitimisho
Kama unavyoweza kuona kwa namna moja ama nyingine processor za Snapdragon ni bora kuliko processor za Mediatek, lakini sio kwamba processor za Mediatek ni mbaya, HAPANA. Processor zote mbili zinaweza kutofautiana uwezo kwenye kila aina ya simu hivyo kuna simu nyingine unaweza ukakuta inayo processor ya Snapdragon lakini ikapitwa kila kitu na simu yenye processor ya Mediatek.Pia kwenye upande wa GPU, sio kila simu yenye processor ya Qualcomm Snapdragon basi moja kwa moja inakuwa inatumia GPU ya Adreno bali zipo simu nyingi zenye kutumia processor hiyo na zinatumia GPU ya ARM Mali, Samsung ni moja ya mfano wa simu zinazokuja na GPU ya Mali kutokana na processor zake za Exynos ambazo pia hutumia GPU za ARM Mali.
Thats it.. Guys hiyo ndio tofauti kati ya processor za Mediatek Helio na Qualcomm Snapdragon, kama kuna mahali popote hujaelewa unaweza kuuliza kupitia sehemu ya moani hapo chini, Mpaka next time endelea kutembelea stepado.blogspot.com kwa habari zaidi za teknolojia .
asante niishie hapo kwa leo 

Comments

Popular posts from this blog

Jinsi ya Kusoma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online

  Jinsi ya Kusoma Meseji za WhatsApp Bila Kuonekana Online Written by Stepado Pascal Ni wazi kuwa katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia kuna sababu nyingi sana ambazo zinaweza kukufanya uwe na uhitaji wa kusoma meseji uliyotumiwa kupitia programu ya WhatsApp bila programu hiyo kuonyesha kama upo “online” au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo. Kupitia makala hii nitaenda kuonyesha njia mpya na rahisi ambayo unaweza kutumia ili kujibu meseji zako za WhatsApp unazotumiwa bila programu ya WhatsApp kuonyesha kama upo online au bila kuonyesha kama umesoma meseji hiyo yaani tiki mbili za blue. Najua kila mtu anaweza kusema najua hiyo lakini nakushauri endelea kusoma makala hii hadi mwisho kwani unaweza kupata maujanja mapya ambayo pengine ulikuwa hujui kwa namna moja ama nyingine. Kama kawaida sipendi kupoteza muda wako mwingi kwa maneno yangu, basi bila kupoteza muda twende tukangalie njia ya kwanza. Njia ya Kwanza Najua kuwa unaweza kusema kuwa unaweza k...

Download Programu ya Microsoft Office 2019 Pro Plus

Download Programu ya Microsoft Office 2019 Pro Plus Written by STepado pascal Ikiwa tunazungumzia programu bora kwaajili ya ofisi ni wazi kuwa programu ya Microsoft Office ni programu bora sana kwako, programu hii inakuja na uwezo mkubwa sana wa kusaidia mtu ambaye anafanya kazi kwenye ofisi, au hata kama wewe ni mwanafunzi programu hii ni bora sana kwako. Kuliona hili leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia sana kuweza kupata programu ya Microsoft Office 2019 Pro Plus, ambayo imesheheni sifa nyingi sana bure bila kulipia gharama yoyote. Kumbuka hili ni toleo la Pro Plus hivyo limesheheni sifa zote za programu ya Microsoft Office. Baadhi ya programu ambazo zipo ndani ya toleo hili ni pamoja na –     Microsoft Word     Microsoft Excel     Microsoft Powerpoint     Microsoft Outlook     OneNote     OneDrive     Microsoft Teams Kwa kuanza ni vyema kufahamu kuwa programu hii ni kwa ajili ya kompyuta za Windows na inafany...

Kuanzia A-Z List zote za Windows CMD Commands

A-Z List 0f Windows CMD Commands  By  Am IT guy STEPADO Zifuatazo ndizo   list zote za Windows CMD commands  ambazo nimezipangilia katika alphabetically CMD commands. Command Prompt  and  CMD Commands  are unknown territories for most of the Windows users, they only know it as a black screen for troubleshooting the system with some fancy commands. repair a corrupted disk, hide certain drives, to create a hacking-like environment, etc. Nini maana ya Command Prompt na CMD Commands? Command Prompt, kwa jina jingine ni  cmd.exe  or  cmd  —   ni  command line amabyo inatumika kutafsiri application  katikaWindows NT family operating systems. Na CMD Commands ni specific set of instructions given to Command Prompt to perform some kind of task or function on your Windows PC. Most of the Windows CMD Commands are used to automate tasks via script  and batch files, perform advanced administrative functi...

Jinsi ya Ku-install Windows 10, 8, 7 na XP Kwenye Simu za Android

 Jinsi ya Ku-install Windows 10, 8, 7 na XP Kwenye Simu za Android Written by STepado Pascal windows kwenye android (1) Kutokana na teknolojia kubadilika sana vile vile hata simu zetu nazo zimekua zikibadilika kila siku, simu zetu zimekuwa zimebadilika kuanzia uwezo, vitu inavyofanya mpaka matumizi ya simu hizo. kuelewa mabadiliko hayo leo Tanzania Tech tunaenda kukuonyesha njia rahisi ya kuinstall Windows 7, Windows 8, Windows 10 pamoja na Windows XP kwenye simu yako ya Android. Kwa kuanza ni vyema ukajua kuwa uwezo wa kutumia Windows kwenye simu yako unaweza kukusaidia wewe kutumia simu yako kama kompyuta, njia hii itakusaidia sana kama simu yako inauwezo wa kutumika kwenye screen kubwa ili kukupa uwezo wa kufanya vitu mbalimbali kama unavyo tumia kwenye kompyuta, yaani bila tofauti kubwa utafauti ni kwenye graphics pekee. Kwa kuanza unatakiwa kuwa na simu yako ya Android yenye RAM at-list GB 1 na kuendelea, uharaka wa kuinstall Windows kwenye simu yako unategemeana sana na Uwezo...

Njia za Kutoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki (Njia Rahisi)

Njia za Kutoa Simu Yako kwenye Hali ya Kustaki (Njia Rahisi) Written by Stepado Pascal Kama wewe ni mmoja wa watu ambao wanakuwa na tatizo la simu yako kustaki mara kwa mara basi makala hii ni kwa ajili yako. Kama unavyojua, simu nyingi za Android za sasa zinakuja zikiwa zimefungwa moja kwa moja na hauwezi kufunguka simu hiyo kwa namna yoyote. Ni kweli kwamba njia rahisi ya kuweza kuondoa simu kwenye hali ya kustaki ni kutoa battery ya simu hiyo na kurudisha, lakini unafanyaje kama simu yako imefungwa moja kwa moja na huwezi kufungua simu hiyo ili kutoa battery...? Majibu ninayo. Kwanza awali ya yote labda nikwambie kuwa, hatizo hili limenikuta binafsi na katika hali ya kufanya ufumbuzi nikaona sio mbaya nikishiriki na wewe njia ambazo nilitumia kuweza kuondoa simu yangu kwenye hali ya kustaki. Kumbuka njia hizi mara nyingi zinafanya kazi kwenye simu za aina zote yaani simu za Android pamoja na simu za iPhone au iOS.Zipo njia nyingi sana lakin katika zote...

Link ya kupata windows

Mambo vp Wana blog ,leo nimekuletea link hii hapa chini ,uweze kupakuwa window yoyote uitakayo kwa matumizi yako ,hvo basi bila kupoteza wakati click hiyo link hapo itakupeleka kupakuwa windows. Ukipata changamoto yoyote niachie comments yako hapo chini au chochote Cha kushare nasi karibu Sana.Tukutane tena wakati mwingine Click hapa

Antivirus ipi Bora zaidi kwa Windows 10?

Welcome in Technology   MAADA LEO *Anti-virus Ipi ni Bora zaidi kwa Windows 10?*  *By Am IT guy STEPADO* Windows 10 haitaingilia kazi mara kwa mara kukutaarifu kupakia ‘Anti-virus’ kwenye mashine yako kama vile Windows 7 ilivyokuwa ikifanya. Hii ni kwa sababu kuanzia Windows 8, Microsoft walifanya uamuzi wa msingi wa kuweka Anti-virus moja-kwa-moja kwenye mfumo wao. Antivirus hii inaitwa Windows Defender na ni Antivirus ambayo Microsoft wenyewe wanaitoa bure pamoja na WIndows mpya. Kwa maana hiyo swali la msingi la makala hii linafaa kubadilika na kuwa – ‘Je Windows Defender ni antivurus ni bora zaidi kwa usalama wa kompyuta yako au la?’ Windows Defender WIndows Defender inatokana na Microsoft Security Essentials (MSE) na ni, kwa maneno mengine, toleo la kisasa zaidi la MSE, ambayo ilikuwa ni antivirus ya bure kabisa kwa ajili ya Windows 7. Kwa sasa, antivirus ya Windows Defender inakuja pamoja na Windows na ni ngome ya kwanza kwa kompyuta yako. *Je, Windows Defender Inatosha...