Njia Rahisi ya Kutengeneza Katuni Kutoka Kwenye Picha
Written by Stepado Pascal
Kama wewe ni mmoja wa watu ambao
wanapenda kubadilisha picha zako kutoka kwenye picha za kawaidia na kuzifanya
kuwa kama katuni basi makala hii ni kwa ajili yako. Tofauti na njia nyingine
ambazo zimezoeleka njia hii ni rahisi sana na unaweza kubadilisha karibia kila
picha kwa urahisi.
Kama unavyoweza kuona, njia hii
inafanya kazi kwa asilimia 100 na utaweza kuona picha hizo mbili ambazo
nimezitoa mtandaoni tu na kuweza kujaribu njia hii rahisi. Kupitia njia hii
huna haja ya kuwa na ujuzi wowote bali unahitaji kuwa na kompyuta tu na kama huna
kompyuta basi unaweza kujaribu njia hii kupitia simu yako ya Android au hata
iOS.Bila kuendelea kupoteza muda zaidi
basi moja kwa moja twende nikuonyesha hatua unazotakiwa kufuata. Kama unayo
kompyuta basi fuata njia za kompyuta na kama huna kompyuta basi fuata njia za kutumia simu.
Tengeneza
Katuni Kwa Kutumia Kompyuta
Kwa kuanza Bofya Hapa, kisha
moja kwa moja pakua programu ya Prima Cartoonizer kwenye kompyuta yako. Kumbuka
wakati unapakuwa programu hiyo chagua sehemu ya Download Prima Cartoonizer EXE file.
Download programu hiyo kwenye kompyuta yako kisha install kwenye kompyuta yako
na sasa washa programu hiyo.
Baada ya kuwasha bofya kitufe cha
Add kilichopo upande wa kulia juu, chagua picha unayotaka kufanya iwe katuni.
Baada ya kuweka picha hiyo angalia upande wa kushoto utaona Sample ya picha
ambazo unaweza kufanya ziwe kama hivyo. Chagua aina ya katuni ambayo
unapendelea zaidi na kisha subiri baada ya muda na utaona picha yako imekuwa
katuni.
Kama unavyoweza kuona hapo juu,
hivyo ndivyo ambayo utaweza kubadilisha picha yoyote kuwa katunia kwa kutumia
kompyuta yako. Baada ya kuridhika na aina ya katuni unaweza kuhifadhi picha
yako moja kwa moja kwa kubofya kitufe cha Save juu katikati.
Tengeneza
Katuni Kwa Kutumia Simu
Kama huna kompyuta usijali pia
unaweza kutumia njia hii kwenye simu yako, iwe unatumia simu ya Android au iOS
utaweza kufanya njia hizi kwa urahisi kabisa. Kwa kuanza unatakiwa kutembelea tovuti hii hapa, baada ya hapo bofya kitufe cha Choose File, kisha chagua
picha unayotaka kubadilisha iwe katuni.
Baada ya hapo subiria kwa muda mfupi
kidogo na utaweza kuona picha imebadilika kabisa na utaweza kuona picha yako
imekuwa katuni kwa haraka na urahisi kabisa.
Kama unavyoweza kuona kwenye picha
hapo juu huo ndio muonekano wa programu hiyo mtandaoni. Kwa sababu mimi
nimetumia kompyuta unaweza kuona muonekano wa tofauti kwenye simu yako lakini
na kuhakikishia utaweza kutengeneza katuni kwa haraka na urahisi bila kutumia
muda mrefu. Natumaini umeweza kutengeneza katuni kwa kutumia simu au kompyuta
yako.
Solutions Tech tumejikita kuhakikisha
hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi.
Comments
Post a Comment